definition for: #ChaguaAmani
1 Definition for Hashtag #ChaguaAmani
1
Tunapoelekea katika maadhimisho ya siku ya amani duniani, September 21, na tunapoelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania, October 25, 2015, tuna kila sababu ya kukumbushana juu ya amani yetu.
Chagua Amani ni kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchagua amani kwa ajili ya Tanzania hasa katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu.
Kampeni hii inawalenga watanzania wote bila kujali itikadi ya chama au dini, na inahamasisha wananchi kutoshabikia siasa ambazo zinaweza kutowesha amani ya nchi yetu.
Kiongozi bora ndiyo amani yetu na maendeleo yetu, ushabiki wa kisiasa utatirudisha nyuma na kutuingiza katika machafuko.
One Action Tanzania inawakaribisha Watanzania wote kuungana nasi kuwakumbusha Watanzania na viongozi wote, kuweka amani ya taifa mbele ya maslahi yao ya kisiasa.

